Mifuko mipya nchini mwetu,mizuri,haina garama.Mifuko hii pia hachafui mazingira.Tukijaribu tutaweza lakini tukumbuke pia kuwa mifuko ya plastiki haiozi,inasababisha madhara mengi,lakini mifuko hii inaweza kutumika kama mbolea pia.
migos-narcos
Masanja Mkandamizaji-NII vedio
Mwanzilishi wa blog hii ni maarufu kwa jina la Rickyllobbe.Anahamasisha maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania.yeye ni mfano wa kuigwa.Napia Jina la blog ya Rickyllobbe lina tamkwa,RICKY-LOB.

Game la mpira bora zaidi ni lipi?, linapatikana wapi?, kwa nini ni bora zaidi?. Endelea kusoma na utapata majibu ya maswali yote hayo kadri unavyoendelea.
Game la mpira bora zaidi ni lipi?
Dream League Soccer(DLS). Kati ya magemu yote ya mpira niliyowahi kucheza katika simu yangu Dream League Soccer ndio game bora zaidi kwa vigezo nilivyokua nimeviweka.Kwa nini DLS ndio game bora zaidi?
Kuna sababu nyingi zinazosababisha nitoe nafasi hii kwa DLS licha ya uwepo wa magemu mengine- Unapata experience ya soka halisi kutokana na uwepo wa wachezaji halisi kabisa. Japo hii inapatikana pia katika games nyingine ila ni moja ya sababu.
- Linahitaji space ndogo(lina mb chache). Hauhitaji nafasi kubwa katika simu yako au kutumia kiasi kikubwa cha kifurushi chako kudownload game hili kutokana na udogo wake. Ni kama mb 300 ukilinganisha na mengine yaliyo na kama gb 1 na kuendelea
- Ni rahisi zaidi katika kucheza. Siongelei urahisi wa mechi bali nazungumzia kuelewa vitu unavyohitajika kufanya kama kununua au kuuza wachezaji na mengine mengi.
- Kuna mtiririko mzima wa mechi kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hapa unaona matukio yote ya mechi ikianza hadi mwisho ukilinganisha na games nyingine ambazo matukio yapo kwa vipande vipande.
Game hili linapatikana wapi?
Sehemu bora zaidi ya kulipata game ili ni kwenye Google PlayStore. Lakini unaweza kulipata kwa kusearch tu internet au sehemu kama uptodown softonic au mobogenie storeKwa nini Google PlayStore?
Kwa sababu unakuwa na uhakika wa kudownload game halisi likiwa full na usalama wa kifaa chako pia ni uhakika. Kwa kutumia njia nyingine unaweza kudownload game nusu na usijue jinsi ya ku install baadae.Nifanyeje ili kupata coins nyingi zaidi?
Njia ya kwanza ni kununua coins hizo kwa pesa halali ndani ya game hilo. Lakini pia kuna njia rahisi ya kufanya hivyo bila kutumia pesa lakini sio halali kuitumia angalia hapaGame hili lina udhaifu gani?
KIla kizuri hakikosi udhaifu. Graphics katika game hili ni za kuridhisha lakini zinazidiw sana na game kama PES. NA pia katika swla la uhalisia wa wachezaji apo FIFA ipo juu zaii ya DLS. KAtika gemu hili pia ni ngumu sana kutafuta hela kwa njia ya kawaida ya game.Sipendi DLS game gani zuri zaidi?
Kama hutopenda chaguo hili napendekeza uchukue FIFA Football au PES Mobile.Angaliazaidi katika https://mojasky.com/game-la-mpira-bora-zaidi-kwa-ajili-ya-simu/
Teknolojia inakua kwa kasi sana. Takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa simu (hususa Android) wamekuwa wengi na wataongezeka kadri siku zinavyozidi kusogea. Hivyo ni vema kuchukua taarifa hizo kama fursa iliyo wazi kwa kila mmoja mwenye ndoto au wazo la kufikia watu wengi.
Taarifa nyingine nzuri ni kuwa mfumo wa android ndio rahisi zaidi kutengeneza apps zake, aidha uwe na ujuzi au usiwe nao kabisa. Kama ungependa kujua jinsi ya kutengeneza app ya android bila kuwa na ujuzi yani programming endelea kusoma post hii. Kama ungependa kujua namna ya kutengeneza app hizo kwa njia ya programming yani Android Studio na nyingine post hii haielezei kuhusu hilo japo unaweza kujifunza mambo kadhaa mbayo ni muhimu pia.
Hatua za kufuata kutengeneza app yako
1.Research (fanya uchunguzi)
Kama unatengeneza app kwa ajili ya biashara ni vizuri ukajua watumiaji watakuwa wa kina nani? watakuwa tayari kulipia? Unatoa huduma ambayo watu wataihitaji? na mengine yanayofanana na hayo
2.Tengeneza app yako
Ukishajua app unayohitaji kuitengeneza unakuja kwenye hatua muhimu kabisa ya kuitengeneza app yako. Njia rahisi ni kwa kutengeneza app online yaani katika website zinazotoa huduma hiyo. Unaweza kutumia njia hizi rahisi.-
Web 2 Apk
Kama unataka kutengeneza app simpo tu kwa ajili ya blog au website yako ili ni chaguo bora. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website yao unaweka website yako na baada ya sekunde kadhaa app yako inakuwa tayari. Hapa hakuna kujiunga ila ni lazima uwe na blog au website kwa ajili ya kutengeneza app yake.
-
Andromo
Unataka kutengeneza app kwa ajili ya Masomo, sauti, ramani, picha, ukurasa wa youtube, blog au website unaweza tumia hii. Unachotakiwa kufanya ni kuingia katika website yao ili kuanza kutengeneza app yako. TanzaniaTech wameeleza hatua jinsi ya kutengeneza app kwa kutumia Andromo hapa
- Appy Pie
- AppMachine
- Mobile Roadie
- BiznessApps
- BuzzTouch
- TheAppBuilder
- Good Barber
- Kinetise
- Como DIY
- App maker
- AppsGeyser
- Jmango
- BuildFire
3.Test app yako
Hii ndiyo hatua inayofurahisha zaidi. Hapa unajaribu app uliyoitengeneza kama inakidhi vigezo na matarajio uliyoyaweka kabla ya kuitengeneza app yenyewe. Kama unatumia pc kutengeneza ni vyema ukawa na simu kwa ajili ya ku test.4.Sambaza app yako
Kama umemaliza hatua zote sasa unaweza kuiweka app yako katika platforms mbalimbali na hata kufanya matangazo kwa ajili ya kupata watumiaji. Unaweza kuiweka Google Play Store (ni muhimu kwa sababu watumiaji wengi wapo hapa), Amazon App Store na nyingine.5.Zaidi
Nitanufaika vipi na kuwa na app?
Ukitengeneza app itakayotumiwa na watu wengi unaweza ingiza kipato kwa kuweka matangazo, kuifanya app ya kulipia (kabla mtu hajadownload) au kuuza vitu au huduma katika app yako.Nawezaje kuiweka app yangu playstore?
Kuweka app playstore unatakiwa kufungua akaunti playstore ambayo inagharimu kiasi cha pesa kinacholipwa mara moja wakati wa kujiunga 25$ – kama Tsh 60,000.Unahitaji kifaa gani simu au kompyuta?
Njia bora ni kwa kutumia kompyuta, lakini inawezekana kwa asilimia 100 kutengeneza kwa kutumia simu.Ni vitu gani vingine vinahitajika?
kwa hatua tajwa hapo juu unahitajika uwe na kifaa chako (simu au kompyuta) na mb za internet angalau MB 500Nitatumia muda gani kutengeneza hiyo app ?
Muda utategemea na uzoefu wako na utayari wa mahitaji yako kabla ya kutengeneza.https://mojasky.com/jinsi-ya-kutengeneza-app-android-application/








